Nenda Kwa Maudhui Moja kwa Moja

Dhamira yetu ni kusaidia watu kuelewa Biblia kama simulizi moja inayoongoza kwa Yesu.

Video

Angalia video zetu zinazochanganua vitabu vya Biblia. Tazama na pakua maudhui kutoka kwenye video zetu.

Kuhusu BibleProject

Kolaji ya picha za timu ya BibleProject: mkutano wa wafanyakazi, msanii akichora, seti ya utayarishaji wa video, na waanzilishi Tim Mackie na Jon Collins.

BibleProject ni shirika lisilo la kibiashara linalofadhiliwa na michango ya umma, lenye makao yake makuu nchini Marekani. Tunatayarisha nyenzo za kuwasaidia watu kuipitia Biblia kama simulizi moja inayoungana inayomwelekeza msomaji kwa Yesu. Lengo letu ni kufanya dhana ngumu za kibiblia ziwe wazi na zenye kufikika kwa wale wenye shauku ya kujifunza zaidi kuhusu Biblia. Tunatayarisha kila kitu tukilikusudia kanisa la ulimwenguni kote, na ingawa wasomi wetu wanatoka katika mapokeo mbalimbali ya Kikristo, wameungana katika azma yao ya kuona watu wengi iwezekanavyo wakiipitia simulizi hiyo moja iliyoungana ya Biblia.

Historia yetu ilianza mwaka 2014 wakati marafiki wa muda mrefu, Dkt. Tim Mackie na Jon Collins, walipounganisha usomi wa kibiblia na sanaa ya simulizi ili kutayarisha video za bure kwa lugha ya Kiingereza za kuwasaidia watu kuielewa Biblia. Tangu wakati huo, BibleProject imekua na kuwa shirika lenye watu zaidi ya 140, na kwa msaada wa wazawa wa lugha na timu mbalimbali duniani kote, imetoa maelfu ya video katika lugha na lahaja zaidi ya 50. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu mtazamo wetu juu ya Maandiko Matakatifu hapa.

Kila kitu tunachotayarisha kinapatikana bila malipo kutokana na jumuiya ya wafadhili wakarimu kama wewe.

Jiunge na BibleProject

Kila kitu tunachotayarisha kinapatikana bila malipo kutokana na jumuiya ya wafadhili wakarimu kama wewe.