Back

Sheria na Masharti ya Matumizi

BibleProject

Yalisasishwa Septemba, 2019

Karibu kwenye BibleProject -- tunafurahia kukuona!

BibleProject inaamini katika kushiriki makala tunayotayarisha na watu na vikundi vingi iwezekanavyo kote ulimwenguni. Tungependa video, mabango, madokezo na maudhui yetu mengine yatumiwe na walimu na viongozi wa kidini bila malipo ili kuendeleza ufahamu na mazungumzo kuhusu Biblia. Sheria na Masharti haya ya Matumizi (wakati mwingine hurejelewa tu kama "Sheria na Masharti") yanatumika kutimiza lengo hilo, huku yakilinda maudhui na sifa yetu dhidi ya matumizi mabaya au yasiyoruhusiwa. Ikiwa ungependa kutumia makala tunayotayarisha, unahitaji kutii Sheria na Masharti haya. Sisi ni shirika lisilo la faida linalosimamiwa chini ya sheria za jimbo la Oregon nchini Marekani, lakini tunajitahidi kuwa na mtazamo wa kimataifa. Kwenye Sheria na Masharti haya, tunajirejelea kama "sisi", "yetu", "TBP", "The Bible Project", au, bila shaka, "BibleProject".

Sheria na Masharti haya, pamoja naIlani yetu ya Faragha, yanadhibiti matumizi yako ya tovuti zetu, vituo na kurasa zetu kwenye mitandao ya kijamii, na huduma yoyote nyingine ya TBP inayopatakana mtandaoni (kwa pamoja zinarejelewa kama "Tovuti"). Tafadhali soma Sheria na Masharti haya kwa makini kabla hujaanza kutumia Tovuti.

 1. Kukubali

 1. Muhtasarii

 1. Kujisajili

 1. Umiliki wa Mali ya Uvumbuzi

 1. Chapa za Biashara za TBP

 1. Matumizi Yako ya Tovuti na Maudhui

 1. Masharti ya Matumizi Yako ya Tovuti na Maudhui

 1. Maudhui ya Mtumiaji

 1. Usalama wa Tovutii

 1. Kubadilisha, Kusimamisha au Kukomesha Utumiaji wa Tovuti

 1. Faragha na Mawasiliano

 1. Sheria Husika

 1. Kusalimisha Haki

 1. Kanusho la Dhima

 1. Kikomo cha Dhima

 1. Kufidia

 1. Kubadilishwa kwa Sheria na Masharti haya

 1. Makubaliano ya Upatanishi

Kukubali

Ili uweze kufikia, kuvinjari, au kutumia Huduma zetu, sharti ukubali kuzingatia kikamilifu Sheria na Masharti haya mradi unatumia Tovuti, Maudhui (yamefafanuliwa hapa chini), au bidhaa au huduma zetu. Usipokubali Sheria na Masharti haya, hutaruhusiwa kutumia Huduma. Kukubali kwako kunachukuliwa kuwa umeingia katika mkataba wa kisheria. Sheria na Masharti yetu yanajumuisha makubaliano yote kati yako na BibleProject kuhusu matumizi yako ya Tovuti na Maudhui na yanatumika kadri inavyoruhiswa kisheria. Kushindwa kwetu kutekeleza kipengee au haki yoyote kwenye Sheria na Masharti yetu hakutachukuliwa kuwa kusalimisha haki au kipengee hicho.

Ikiwa una maswali au maoni yoyote kuhusu Sheria na Masharti haya, tafadhali wasiliana nasi kwenye webmaster@jointhebibleproject.com au utupigie simu bila malipo kupitia nambari (855) 700-9109.

Muhtasarii

BibleProject si sehemu ya dhehebu au kikundi maalum cha Kikristo. Tunatumai kuwa watu wote watanufaika kutokana na kazi yetu, bila kuzingatia misimamo yao ya kidini au isiyo ya kidini. Lengo letu si kuendeleza mafundisho mahsusi ya dhehebu lolote maalum la Kikristo, bali kuchambua mafundisho na dhana za kitheolojia zinazotokana na usomaji wa matukio kwenye Biblia kwa kuzingatia kwa kina muktadha wa kihistoria na kitamaduni. Wakati mwingine, huenda tukachambua vifungu vya Biblia kwa njia inayodhihirisha imani na msimamo wetu wa kidini, lakini lengo letu kuu ni kwamba simulizi na mafundisho kwenye Maandiko yajisimamie.

Kwa sababu tumejitolea kufasiri biblia kwa njia patanishi na pia kuteua nyenzo na mbinu za kazi hiyo ya ufasiri, hatungependa watu wafasiri Maudhui yetu visivyo kwa kutozingatia muktadha husika. Pia, kwa sababu sisi ni shirika lisilo la faida, haturuhusu mtu binafsi au shirika lolote kujinufaisha kutokana na matumizi yao ya Maudhui yetu. Kujaribu kujinufaisha na Maudhui yetu, au kutumia Maudhui yetu kwa njia yoyote inayobadilisha ujumbe, hitimisho, kauli au yaliyomo kwenye Maudhui, kunakiuka Sheria na Masharti haya na kutakuondolea haki yako ya kutumia Maudhui.

Sheria na Masharti haya yanatumika katika utumiaji wako wa video zetu, mabango, madokezo, podikasti, rekodi zingine za sauti, maudhui na vipengele vingine vyovyote vinavyopatikana kwenye Tovuti yetu, kama vile bibleproject.com, na pia utumiaji wa maudhui yoyote kama haya katika kurasa zetu kwenye mitando ya kijamii au kurasa zetu za utiririshaji wa maudhui, kama vile vituo vyetu kwenye YouTube na Vimeo (kwa pamoja zinarejelewa kama "Maudhui"). Maudhui hayapaswi kutumika vinginevyo isipokuwa kama ilivyobainishwa katika Sheria na Masharti haya. Kwa kiwango ambacho kampuni zingine zinatoa huduma za upangishaji au huduma zingine kwa TBP (kwa pamoja zinarejelewa kama, "Watoa Huduma"), na sheria na masharti ya Watoa Huduma hao yanatumika katika tovuti, vituo, kurasa kwenye mitandao ya kijamii au kwingineko mtandaoni ambapo Maudhui yanapatikana, Sheria na Masharti haya yatatumika pamoja na sheria na masharti hayo.

Ili uweze kufikia, kuvinjari au kutumia Tovuti au Maudhui, sharti ukubali kuzingatia kikamilifu Sheria na Masharti haya. Usipokubali Sheria na Masharti haya, hutaruhusiwa kutumia Maudhui, Tovuti, huduma au kipengele chochote wanachotoa.

Kujisajili

Tovuti yetu inakupa maelezo ya jumla kuhusu mipango na huduma za TBP. Unaweza kujisajili nasi kupokea majarida na maelezo mengine, kutoa mchango au kununua mtandaoni, kufikia au kutumia Maudhui fulani, au kufikia na kutumia vipengele vingine kwenye Tovuti, vyote hivi kwa mujibu wa Sheria na Masharti haya. Kwa kujisajili nasi, unakubali kwamba (a) unaweza na una idhini na ruhusa ya kuingia katika mkataba na TBP; (b) maelezo ya kibinafsi utakayotoa ni ya kweli, sahihi na kamili; na (c) utatumia tu kitambulisho tutakayokupa kufikia kurasa unazoruhusiwa kwenye Tovuti. Ikiwa TBP ilikuondolea awali idhini ya kufikia Tovuti kwa sababu yoyote, huenda hutaweza kabisa kufikia au kutumia Tovuti.

Ukijisajili nasi, utawajibikia masuala yote kuhusu akaunti na nenosiri lako (ikiwemo kudumisha usiri wao) na akaunti yako kutumiwa na wengine kwa idhini yako au bila idhini yako. Unakubali kuhakikisha kuwa watumiaji wengine wa akaunti yako watazingatia Sheria na Masharti haya. BibleProject haitawajibikia hasara yoyote inayotokana na utumiaji wa akaunti yako kwa njia isiyoidhinishwa.

Sharti utuarifu mara moja kuhusu ukiukaji wowote wa usalama au utumiaji usioidhinishwa wa akaunti yako kwa kutuma barua pepe kwa webmaster@jointhebibleproject.com mada ikiwa "Utumiaji Usioidhinishwa". Hata ukituarifu, utawajibikia shughuli zozote zinazohusishwa na vitambulisho vyako vya ufikiaji, ikijumuisha utozaji wowote unaotokana na utumiaji wa akaunti yako. Tuna haki, kwa hiari yetu, ya kuondoa idhini yako ya kufikia Tovuti au huduma yoyote husika wakati wowote, bila kukuarifu.

Umiliki wa Mali ya Uvumbuzi

Hakimiliki, chapa za biashara na haki zingine za mali ya uvumbuzi kwenye Maudhui na maelezo mengine yoyote yaliyojumuishwa kwenye Tovuti ikiwemo, bila kikomo, programu, maandishi, michoro, nembo, aikoni za vitufe, picha, klipu za sauti, klipu za video, uchakataji na ukusanyaji wa data, utayarishaji na muundo wa jumla wa Tovuti (kwa pamoja zinarejelewa kama, "Mali ya Uvumbuzi"), zinamilikiwa au zimepewa leseni na TBP, na tuna haki zote kuhusiana na Mali ya Uvumbuzi.

Chapa za Biashara za TBP

Japo hakimiliki za Maudhui fulani zimepewa leseni chini ya Sheria na Masharti haya kwa matumizi fulani mahsusi, hujapewa chapa yoyote ya biashara au leseni yoyote ya huduma chini ya Sheria na Masharti haya. Hii inamaanisha kuwa huruhusiwi kutumia jina letu, nembo, au kitambulishi kingine chochote cha TBP kwa njia yoyote isiyoruhusiwa kama matumizi ya haki ya marejeleo chini ya sheria ya Marekani. Hii ni ili kuondoa tashwishi kuhusu uhusiano kati ya TBP na watumiaji wa Maudhui yetu, kwa mfano kushawishika kuwa TBP inaidhinisha au inatoa udhamini kwa mtu anayetumia tu Maudhui kwa mujibu wa Sheria na Masharti haya, na sio chini ya makubaliano tofauti. Ikiwa ungependa kutumia chapa zetu zozote za biashara zaidi ya matumizi ya haki ya marejeleo, tafadhali wasiliana nasi ili uwasilishe ombi la kupewa leseni ya matumizi maalum. Leseni hizo hazipatikani mara kwa mara, lakini zinaweza kutolewa katika hali fulani za kipekee. Leseni ya kutumia vitambulishi vyetu vyovyote inaweza kutolewa tu kupitia makubaliano rasmi ya leseni yaliyoandikwa na kutiwa saini na mmoja wa maafisa wetu walioidhinishwa kihalali. Hakuna mtu mwingine au wakala aliyeidhinishwa kutoa haki yoyote au kuidhinisha utumiaji wa vitambulishi vyetu vyovyote, na idhini, ahadi au mwongozo wowote kama huo ni batili.

Matumizi Yako ya Tovuti na Maudhui

Kama mtumiaji wa Tovuti, una idhini inayoweza kubatilishwa, isiyoweza kuhamishwa, isiyo ya kipekee ya kufikia Tovuti, kuangalia maelezo yaliyo kwenye Tovuti na kutumia Tovuti kama ilivyobainishwa katika Sheria na Masharti haya. Kwa kutumia Tovuti, pamoja na huduma yoyote shirikishi inayohitaji utoe maelezo, unakubali na unathibitisha kwamba (a) maelezo yoyote utakayotoa kwenye Tovuti ni sahihi na ya ukweli; (b) utadumisha usahihi wa maelezo hayo; na (c) matumizi yako ya Tovuti hayakiuki sheria, kanuni au masharti yoyote husika. Maelezo yoyote utakayotoa yatatumika pia kwa mujibu wa Ilani yetu ya Faragha.

Huruhusiwi kutumia Tovuti kwa madhumuni yoyote ya kibiashara au yasiyo halali au yasiyofaa. Unakubali kutotumia, kutokodisha, kutosambaza, kutotoa nakala, kutofichua, kutochapisha, kutouza, kutokabidhi, kutopangisha, kutotoa kijileseni au kutohamisha Tovuti, au sehemu au kipengee chochote husika (ikijumuisha Maudhui) vinginevyo isipokuwa kama ilivyoidhinishwa kwenye Sheria na Masharti haya. Unakubali pia kutonakili, kutofanya utafiti wa kihandisi, kutotafsiri, kutohamisha au kutounda miigo ya Tovuti, au sehemu yoyote ya Tovuti. Uvamizi wa Tovuti, kutekeleza shughuli za ulaghai kwenye Tovuti na shughuli zingine zote zisizo halali ni marufuku na mkiukaji anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria.

Maudhui ya Video. Unaweza kupakua baadhi ya video zetu kwenye tovuti yetu ya www.bibleproject.com au katika vituo vyetu kwenye YouTube (https://www.youtube.com/user/jointhebibleproject au Vimeo (https://vimeo.com/channels/1241213) au kwenye vituo vingine kama hivi tutakavyofungua baadaye (kwa jumla zinarejelewa kama, "Maudhui ya Video"). Unaruhusiwa kupachika mitiririko ya, au viungo vya, Maudhui yetu yoyote ya Video kwenye tovuti yako au programu yako ya simu isipokuwa na hadi pale tutakapokuagiza uiondoe, lakini tu mradi unatii kikamilifu Sheria na Masharti na, hasa, masharti yafuatayo:

 • Huruhusiwi kudai malipo, kujichumia mapato kwa njia isiyo ya moja kwa moja au kuwaomba watumiaji wa tovuti au programu yako kuchukua hatua yoyote ili waweze kufikia Maudhui ya Video.

 • Huruhusiwi kuuza wala kusambaza nakala za Maudhui ya Video.

 • Sharti uweke notisi bainifu na inayoonekana, karibu na Maudhui ya Video, inayotambulisha BibleProject kuwa mtayarishaji na mmliki wa Maudhui ya Video na ijumuishe kiungo cha kuelekeza kwenye www.bibleproject.com ili kuwawezesha watazamaji kutembelea tovuti na kupata maelezo zaidi kuhusu BibleProject.

 • Huruhusiwi kurekebisha au kubadilisha Maudhui yoyote ya Video kwa njia yoyote ile, wala huruhusiwi kuunda miigo ya Maudhui ya Video.

 • Huruhusiwi kupakia Maudhui yoyote ya Video kwenye seva mpya au huduma ya utiririshaji kando na tunazotoa.

Mabango.  Unaweza kupakua baadhi ya mabango yetu kwenye tovuti yetu ya www.bibleproject.com (kwa pamoja yanarejelewa kama, "Mabango"). Unaruhusiwa kupakua, kutoa nakala na kuonyesha Mabango yetu yoyote, kidijitali au kwa njia ya karatasi, isipokuwa na hadi tutakapoondoa ruhusa hii, mradi tu uzingatie kikamilifu Sheria na Masharti haya na hasa, masharti yafuatayo:

 • Huruhusiwi kudai malipo, kujichumia mapato kwa njia isiyo ya moja kwa moja au kuwaomba watu/kampuni zingine kuchukua hatua yoyote ili waweze kuangalia Mabango, wala huruhusiwi kuuza nakala za Mabango.

 • Unaruhusiwa kutoa na kusambaza hadi nakala 500 za karatasi kwa kila Bango tofauti, mradi uzingatie masharti ya mauzo yaliyotajwa hapo juu, hivyo Mabango yote yanasambazwa bila malipo. (Ikiwa ungependa kutoa nakala 500 au zaidi za Bango, tafadhali wasiliana nasi ili uwasilishe ombi la kupewa leseni maalum.)

 • Huruhusiwi kurekebisha au kubadilisha Bango lolote kwa njia yoyote ile, wala huruhusiwi kuunda miigo ya Mabango.

 • Sharti uweke notisi bainifu na inayoonekana, karibu na Mabango yoyote unayoonyesha kidijitali, inayotambulisha BibleProject kuwa mtayarishaji na mmliki wa Mabango na ijumuishe kiungo cha kuelekeza kwenye www.bibleproject.com ili kuwawezesha watazamaji kutembelea tovuti na kupata maelezo zaidi kuhusu BibleProject.

Endapo tutaondoa idhini hii, sharti uondoe Mabango yote unayoonyesha kidjitali, na usitishe usambazaji wa nakala za karatasi za Mabango yoyote.

Maudhui Mengine ya Picha.  Kando na mabango, unaweza kupakua madokezo yetu, hati na maudhui mengine ya picha yasiyobadilika kwenye tovuti yetu ya www.bibleproject.com (kwa pamoja yanarejelewa kama, "Maudhui Mengine ya Picha"). Unaruhusiwa kupakua, kutoa nakala na kuonyesha Maudhui yoyote Mengine ya Picha, kidijitali au mara moja kwa njia ya karatasi, isipokuwa na hadi tutakapoondoa ruhusa hii, mradi tu uzingatie kikamilifu Sheria na Masharti haya na hasa, masharti yafuatayo:

 • Huruhusiwi kudai malipo, kujichumia mapato kwa njia isiyo ya moja kwa moja au kuwaomba watu/kampuni zingine kuchukua hatua yoyote ili waweze kuangalia Maudhui Mengine ya Picha, wala huruhusiwi kuuza nakala za Maudhui Mengine ya Picha.

 • Huruhusiwi kutoa nakala za Maudhui Mengine ya Picha kwa njia ya karatasi.

 • Huruhusiwi kurekebisha au kubadilisha Maudhui Mengine ya Picha kwa njia yoyote ile, wala huruhusiwi kuunda miigo ya Maudhui Mengine ya Picha.

 • Sharti uweke notisi bainifu na inayoonekana, karibu na Maudhui Mengine yoyote ya Picha unayoonyesha kidijitali, inayotambulisha BibleProject kuwa mtayarishaji na mmiliki wa Maudhui Mengine ya Picha na ijumuishe kiungo cha kuelekeza kwenye www.bibleproject.com ili kuwawezesha watazamaji kutembelea tovuti na kupata maelezo zaidi kuhusu BibleProject.

Endapo tutaondoa idhini hii, sharti uondoe Maudhui Mengine yote ya Picha unayoonyesha kidjitali, na usitishe usambazaji wa nakala za karatasi za Maudhui Mengine ya Picha.

Podikasti. Unaweza kutiririsha baadhi ya podikasti zetu na maudhui mengine ya sauti kwenye tovuti yetu ya www.bibleproject.com na kwenye baadhi ya huduma zingine zilizoidhinishwa za utiririshaji wa maudhui ya sauti (kwa pamoja yanarejelewa kama, "Maudhui ya Sauti"). Japo unaruhusiwa kucheza Maudhui yetu ya Sauti unapohitaji kwenye tovuti yetu au huduma zilizoidhinishwa kama vile Apple Podcasts, Google Podcasts, na Spotify (mradi uzingatie masharti yoyote ya huduma hizo zilizoidhinishwa), huruhusiwi chini ya Sheria na Masharti haya kurekodi, kutoa nakala, kutangaza upya au kutumia Maudhui yetu ya Sauti kwa njia nyingine yoyote. Ikiwa ungependa kutumia Maudhui yetu ya Sauti vinginevyo kando na inavyoruhusiwa hapa juu, tafadhali wasiliana nasi ili uwasilishe ombi la kupokea leseni maalum ya matumizi.

Masharti ya Matumizi Yako ya Tovuti na Maudhui

Kufikia Tovuti hakukuruhusu kutumia Maudhui yoyote kwa njia nyingine kando na inavyoruhusiwa kwenye Sheria na Masharti haya. Bila kuweka kikomo kwa yaliyotangulia, isipokuwa iwe imeruhusiwa kwenye Sheria na Masharti haya, huruhusiwi katika hali yoyote:

 • Kuondoa, kubadilisha, kukwepa, kukatiza au kuepuka hakimiliki yoyote, chapa ya biashara au notisi zingine za umiliki zilizo kwenye Maudhui au udhibiti wa haki zozote za kidijitali au kanuni zingine za ulinzi wa Maudhui moja kwa moja au kupitia njia zingine;

 • Kutuma maudhui, kufremu, kuchopoa au kusanidi viungo mbadala vya kipengee chochote cha Tovuti au kufikia Maudhui yoyote kupitia teknolojia au mbinu nyingine kando na tunayotoa au kuidhinisha;

 • Kufikia Tovuti kupitia mfumo wowote wa kiotomatiki, ikijumuisha, lakini sio tu, kwa kutumia "roboti," "programu za kutambaa," "visomaji vya nje ya mtandao," nk., wala kuchukua hatua yoyote inayosababisha au ambayo huenda ikasababisha (kama tutakavyobaini kwa hiari yetu), shughuli nyingi au zisizo adilifu kwenye mfumo wetu;

 • Kupakia data batili kimakusudi au bila kutarajia au kupakia virusi, vidudu dijitali, programu danganyifu, vidadisi au programu zingine hasidi, ziwe hatari au la, kwenye Tovuti, au kuvuruga, kuharibu, kukomesha, kushambulia, kutumia au kupenya mfumo au mtandao wetu, au vinginevyo kuvuruga au kuhatarisha mfumo au usalama wa BibleProject au mitandao yoyote iliyounganishwa, au kuchukua hatua yoyote kuvuruga uendeshaji wa kawaida wa Tovuti na kumzuia mtu au huluki yoyote kuitumia;

 • Kukwepa masharti yanayotumika kuzuia au kuweka vikwazo vya kufikia au kutumia Tovuti, kama vile kwa kudukiza kurasa zinazolindwa au zisizotolewa kwa umma kwenye Tovuti au kukwepa huduma yoyote ya kuzuia utambuzi wa mahali;

 • Kutumia Tovuti kukusanya Maelezo yoyote ya Kibinafsi, ikijumuisha majina ya akaunti na anwani za barua pepe, au kutumia Tovuti kwa madhumuni yoyote ya kujinufaisha kibiashara, bila idhini yetu iliyoandikwa na kutolewa mapema; au

 • Kujaribu kufanya utafiti wa kihandisi wa kipengee chochote cha Tovuti au kujaribu kuchopoa msimbo wa usanidi (ikijumuisha zana, mbinu, michakato na mfumo) unaotumika au unaoendesha Tovuti, kuunda miigo ya kazi au nyenzo za aina yoyote ukitumia Maudhui, iwe unanuia kutoa miigo hiyo ya kazi bila malipo au la, au vinginevyo kukuza biashara kwa kutumia kipengee chochote cha Tovuti.

Ruhusa zilizofafanuliwa kwenye Sheria na Masharti haya zitaondolewa kiotomatiki ukikiuka mojawapo ya kipengee cha Sheria na Masharti haya. Utumiaji wowote wa Maudhui usioruhusiwa kwenye Sheria na Masharti haya huenda ukakiuka sheria za chapa ya biashara au hakimiliki, na, matumizi yoyote bila idhini iliyoandikwa na kutolewa mapema na BibleProject, yamepigwa marufuku.

Maudhui ya Mtumiaji

Iwapo na kadri TBP inavyoruhusu maudhui ya mtumiaji, huenda ukaruhusiwa kuchapisha, kutuma, kuwasilisha au vinginevyo kuchapisha maoni, picha au maudhui mengine kwenye Tovuti ("Maudhui ya Mtumiaji") yanayoweza kufikiwa na kutazamwa na watu wote. Kuhusu Maudhui yoyote ya Mtumiaji utakayochapisha, unakubali kuwa (i) ulitayarisha na unamiliki haki za maudhui au umeruhusiwa na mmiliki kuchapisha maudhui hayo, na (ii) maudhui hayakiuki haki za mtu au huluki nyingine yoyote (ikiwemo, lakini sio tu, hakimiliki, chapa za biashara au haki za faragha) au hayakiuki sheria, kanuni au masharti yoyote husika, Sheria na Masharti haya au yoyote kati ya sera zetu zingine tulizochapisha. Vilevile, Maudhui ya Mtumiaji hayapaswi:

 • Kujumuisha maudhui yoyote ya uongo, ya kudhalilisha, ya kudunisha, chafu, ya kunyanyasa, ya kutishia, yanayobagua, yanayokandamiza, yanayoeneza chuki, yenye vurugu, yanayotumia lugha chafu, potovu, ya ponografia au ya kukera, yasiyofaa, haribifu, yanayokiuka sheria, ya kuvuruga au hatari;

 • Kukiuka haki za kisheria za TBP au za wengine, kujumuisha maudhui yoyote yanayoweza kusababisha dhima ya jinai au kiraia chini ya sheria au kanuni husika au vinginevyo kueneza, kutetea au kusaidia katika kutekeleza shughuli yoyote isiyo halali au inayokiuka sheria;

 • Kumdhuru au kumtishia mtu yeyote au kupoteza au kuharibu mali;

 • Kujumuisha Maelezo ya Kibinafsi ya mtu mwingine, kama vile anwani yake, nambari ya simu, anwani ya barua pepe, nambari ya usalama wa jamii, maelezo ya kifedha, au maelezo mengine yoyote yanayoweza kutumiwa kufuatilia, kuwasiliana au kuiga mtu huyo;

 • Kukiuka hataza yoyote, chapa ya biashara, siri ya biashara, hakimiliki, mkataba, mali nyingine ya uvumbuzi au haki zingine za umiliki za BibleProject au mtu mwingine yeyote;

 • Kuwadhuru au kuwanyanyasa watoto kwa kuwaonyesha maudhui yasiyofaa, kuomba Maelezo ya Kibinafsi au vinginevyo;

 • Kutoa maelezo yasiyo sahihi kuhusu utambulisho wako au uhusiano wako na mtu au shirika lolote, ikijumuisha BibleProject;

 • Kukusanya anwani za barua pepe za wengine, majina ya watumiaji au manenosiri kupitia njia yoyote kwa madhumuni yoyote;

 • Kutuma barua pepe za kusambazwa, barua pepe nyingi au za taka, iwe kiotomatiki au la, au kukatiza, kuvuruga au kuendesha shughuli nyingi zisizotakikana kwenye TBP au mitandao au huduma zilizounganishwa kwenye Wavuti, au kusanikisha au kujaribu kusakinisha au kusambaza vidadisi, programu hasidi au msimbo mwingine wa kompyuta kwenye kompyuta au vifaa vya watu wengine;

 • Kuhusika katika shughuli za kibiashara kama vile mashindano, bahati nasibu, au matangazo mengine ya mauzo, kubadilishana bidhaa, matangazo au ofa za mauzo au ununuzi wa bidhaa na huduma; au

 • Kuwa yenye utata au yasiyofaa familia kama inavyobainishwa na TBP kwa hiari yetu.

Tafadhali chagua kwa uangalifu maelezo unayochapisha kwenye Wavuti na unayoshiriki na watumiaji wengine. TBP inakuhimiza usichapishe kwa umma jina lako kamili, nambari ya simu, anwani ya mtaa, anwani ya barua pepe au maelezo mengine yanayokutambulisha au yanayowezesha watu wasiokujua kukupata au kuiba utambulisho wako. Utawajibikia kikamilifu Maudhui yako ya Mtumiaji na hatua zinazoandamana na kuchapisha maudhui hayo mtandaoni. Utawajibikia hatari zote zinazohusishwa na kuwasiliana na watumiaji wengine kupitia Tovuti, na kadri inavyoruhusiwa kisheria, hatutawajibikia madai au dhima yoyote inayohusiana na Maudhui yoyote ya Mtumiaji yaliyochapishwa kwenye Tovuti na pia hatutawajibikia madai yoyote kuhusiana na vitendo vya watumiaji wengine.

Tuna haki, lakini sio wajibu wetu, kufuatilia, kukagua, kuchunguza, kuchapisha, kuondoa, kukataa, kubadilisha au kuhifadhi Maudhi ya Mtumiaji wakati wowote kwa sababu yoyote bila kukuarifu. Pia tuna haki ya kuchukua hatua yoyote kuhusiana na mizozo kati yako na mtumiaji mwingine yeyote na hatutawajibikia mawasiliano au migogoro yoyote kati yako na watumiaji wengine kutokana na kitendo kilichotekelezwa au ambacho hakikutekelezwa na mtumiaji. Utawajibikia kikamilifu vitendo vyako kwenye Tovuti na mawasiliano yako na watumiaji wengine.

Tunaweza kukataa, kubadilisha au kuondoa Maudhui ya Mtumiaji bila kukuarifu kutokana na sababu yoyote kwa hiari yetu, ikijumuisha tunapobaini kuwa Maudhui ya Mtumiaji huenda yakakiuka Sheria na Masharti haya au yana utata. Hatupendekezi Maudhui yoyote ya Mtumiaji na Maudhui ya Mtumiaji yaliyochapishwa hayaonyeshi misimamo, mitazamo au mawaidha yetu. Hatuwajibikii dhima kwa Maudhui yoyote ya Mtumiaji ambayo wewe au watu wengine wanachapisha au kutuma kwenye au kupitia Tovuti, wala hatuwajibikii kitendo cha moja kwa moja au kisicho cha moja kwa moja kuhusu kutuma, mawasiliano au maudhui yanayotolewa na mtumiaji yeyote au mtu mwingine.

Usalama wa Tovuti

Huruhusiwi kabisa kukiuka au kujaribu kukiuka vipengele vya usalama kwenye Tovuti, kama vile kwa:

 • Kufikia data ambayo hupaswi kufikia au kuingia kwenye seva au akaunti ambayo huna idhini ya kufikia;

 • Kujaribu kuchunguza, kutafuta au kufanya jaribio ili kugundua udhaifu wa mfumo au mtandao, au kukiuka usalama au hatua za uthibitishaji isipokuwa iwe tumekuruhusu kufanya hivyo kwa kukuandikia idhini;

 • Kujaribu kukatiza huduma ya mtumiaji, seva pangishi au mtandao wowote, kama vile kupitia kupakia virusi, kupakia data nyingi mno, kuendesha shughuli zisizotakikana, kutuma taka, kutuma barua pepe nyingi au kusababisha hitilafu; au

 • Kutuma barua pepe ambazo wapokeaji hawajaomba kutumiwa, ikijumuisha ofa na/au kutangaza bidhaa au huduma kwa kuiga kitambulishi cha kifurushi cha TCP/IP au sehemu yoyote ya maelezo ya kitambulishi katika barua pepe au chapisho lolote kwenye kikundi cha majadiliano cha mtandaoni.

Unakubali kuwa hutatumia kifaa chochote, programu au shughuli mahsusi kukatiza au kujaribu kukatiza uendeshaji wa kawaida wa Tovuti au shughuli yoyote inayotekelezwa kwenye Tovuti. Unakubali pia kuwa hutatumia au hutajaribu kutumia mtambo, programu, zana, kipengele, kifaa au huduma nyingine yoyote (ikijumuisha vivinjari, programu za kutambaa, roboti, programu fiche au vidadisi) kuvinjari au kutafuta kwenye Tovuti kando na mtambo wa utafutaji na huduma za utafutaji tunazotoa kwenye Tovuti hii na kando na vivinjari vya watu wengine vinavyopatikana kwa umma kama vile Chrome, Firefox, Safari au Edge.

Ukikiuka masharti ya usalama wa mfumo au mtandao wetu, utawajibikia dhima ya jinai au kiraia. Tutachunguza matukio yanayohusishwa na ukiukaji huo. Tunaweza kuhusisha au kushirikiana na mamlaka husika za kutekeleza sheria katika kuwashtaki watumiaji wanaohusika katika ukiukaji huo.

Kubadilisha, Kusimamisha au Kukomesha Utumiaji wa Tovuti

Tuna haki ya kubadilisha, kusitisha au kuondoa kipengee chochote cha Tovuti wakati wowote na mara kwa mara, kwa hiari yetu na bila kukuarifu au kuwajibikia dhima, ikiwemo kuongeza au kuondoa vipengele fulani au kufunga Tovuti yote. Mara kwa mara, tunaweza kuzuia ufikiaji wa baadhi ya kurasa au Tovuti yote. Pia tuna haki ya kusimamisha au kufunga akaunti yako au kukuzuia kufikia au kutumia Tovuti, bila kukujulisha au kuwabijikia dhima, kwa sababu yoyote au bila sababu yoyote kwa hiari yetu. Ipasavyo, kwa sababu yoyote, na bila kukuarifu, sehemu yoyote ya Tovuti au Tovuti yote inaweza kukosa kupatikana wakati wowote na kwa kipindi chochote.

Tukisimamisha au tukiondoa kipengee chochote cha Tovuti au tukifunga akaunti yako, hatutawajibikia kukupa maelezo au maudhui yoyote. Tunaweza pia kufuta mapendeleo yako au mambo mengine yanayokuvutia yaliyohifadhiwa au yanayohusishwa na akaunti yako. Huna haki ya kuwasilisha madai kuhusiana na maelezo yoyote tutakayofuta bila kuzingatia umuhimu wa maelezo hayo kwako, na tunakanusha umuhimu wa maelezo yako yoyote yaliyohifadhiwa kwenye seva zetu.

Faragha na Mawasiliano

Ilani ya Faragha.  Unathibitisha kuwa umesoma na kuelewa Ilani yetu ya Faragha. Unaweza kupitia Ilani yetu ya Faragha wakati wowote.

Idhini ya Mawasiliano ya Kielektroniki.  Unakubali kupokea mawasiliano kutoka kwetu kielektroniki, kupitia barua pepe, notisi inayochapishwa kwenye Tovuti, au njia nyingine ya kielektroniki, kama tutakavyobaini kwa hiari yetu. Unakubali kuwa masharti yoyote ya kukutumia notisi, ufumbuzi, makubaliano au mawasiliano mengine ya kuandikwa yametimizwa na mawasiliano hayo ya kielektroniki. Hatuwajibikii uchujaji wowote wa kiotomatiki ambao wewe au mtoa huduma zako za mtandao atatekeleza kwenye mawasiliano hayo ya kieletroniki.

Ufikiaji wa Maelezo Yako kupitia Watu Wengine. Unapojisajili kupokea au kutumia bidhaa na huduma zetu, unaweza kutupatia idhini ya kufikia maelezo yako yaliyokusanywa na watu wengine. Kwa mfano, unaweza kuunganisha akaunti yako ya Facebook, hivyo kutuwezesha kupata maelezo kutoka kwenye akaunti hizo (kama vile jina lako kamili na anwani yako ya barua pepe). Maelezo tunayopata kutoka kwenye huduma hizo mara nyingi hutegemea mipangilio yako au ilani zao za faragha, kwa hivyo hakikisha umekagua mipangilio yako.

Sheria Husika

BibleProject inadhibiti na kuendesha Tovuti kutoka kwenye ofisi zake zinazopatikana Marekani. Madai kuhusiana na, ikijumuisha matumizi ya, Tovuti na maudhui yaliyo hapa ndani yanasimamiwa na sheria za Marekani na Jimbo la Oregon. Ukichagua kufikia Tovuti ukiwa katika eneo lingine, unafanya hivyo kwa hiari yako na utahitajika kuzingatia sheria husika za eneo hilo.

Kanusho la Dhima

BibleProject INATOA TOVUTI NA MAUDHUI YAKE "KAMA YALIVYO" NA HAITOI THIBITISHO AU DHIMA YA AINA YOYOTE, IWE DHAHIRI AU KWA KUDOKEZA, IKIJUMUISHA, LAKINI SIO TU, DHIMA AU MASHARTI KUHUSU VIFUNGU VILIVYOREJELEWA AU THIBITISHO LA UTIIFU AU UFAAFU KWA MADHUMUNI MAALUM, AU KUTOKIUKA MASHARTI YA MAUDHUI NA UENDESHAJI NA WA TOVUTI. JAPO TBP INACHUKULIA MAUDHUI KUWA SAHIHI, KAMILI NA YALIYOSASISHWA, TBP HAITHIBITISHI AU KUTOA HAKIKISHO KUWA MAELEZO YANAYOPATIKANA KWENYE TOVUTI NI SAHIHI, KAMILI AU YALIYOSASISHWA. TBP HAITHIBITISHI UPATIKANAJI WA TOVUTI ZETU NA HATUKUAHIDI CHOCHOTE KUTOKANA NA MATUMIZI YAKO YA TOVUTI ZETU. TAHADHARI UNAPOTUMIA TOVUTI ZETU.

Hatuwajibikii na hatutoi dhima yoyote, kwa njia dhahiri au kwa kudokeza, ya maudhui yoyote kwenye tovuti yetu, ikijumuisha, lakini sio tu, kuhusiana na usahihi na kutegemeka kwa maudhui yoyote yaliyochapishwa kwenye au kupitia tovuti yetu, iwe imetekelezwa nasi, wakala wetu, wawakilishi, watumiaji wetu, kwa kutumia kifaa au huduma yoyote inayohusishwa au inayotumiwa na tovuti yetu au vinginevyo. Huenda tovuti zetu zina viungo vya kuelekeza kwenye tovuti zingine, na hatuwajibikii maudhui, usahihi au maoni kwenye tovuti hizo zingine, na hatuchunguzi, hatufuatilii wala kuangalia tovuti hizo ili kukagua usahihi au ukamilifu. Kujumuisha tovuti iliyounganishwa kwenye tovuti yetu hakumaanishi kuwa tumeidhinisha au tunapendekeza tovuti hiyo. Tahadhari unapovinjari tovuti hizo za watu wengine. Hutuwajibikii matangazo au programu za watu wengine zinazochapishwa kwenye au kupitia tovuti yetu, wala hatuwajibikii bidhaa na huduma zinazotolewa na watangazaji hao. Hatuwajibikii upungufu au kitendo chochote (iwe mtandaoni au nje ya mtandao) cha mtumiaji yeyote wa tovuti zetu ikijumuisha chapisho lolote la mtumiaji kwenye tovuti yetu. Hatuwajibikii hitilafu, upungufu, usumbufu, ufutaji, kasoro, ucheleweshaji katika uendeshaji au kutuma, hitilafu ya huduma ya mawasiliano, wizi, uharibifu, ufikiaji usioidhinishwa, au kubadilishwa kwa mawasiliano yoyote ya mtumiaji. Hatuwajibikii matatizo, uharibifu, kasoro au hitilafu zozote zinazohusiana na tovuti zetu au utumiaji wako (ikijumuisha zinazotokana na au kupitia huduma au mtandao wa mawasiliano, mifumo ya kompyuta ya mtandaoni, virusi au programu zingine hasidi, seva au watoa huduma, vifaa vya kompyuta, programu, hitilafu ya kutuma barua pepe yoyote kutokana na matatizo ya kiufundi au shughuli nyingi mno kwenye Intaneti na/au kwenye tovuti zetu). Hatutawajibikia uharibifu au hasara yoyote, ikijumuisha mtu kujeruhiwa au kufariki, kutokana na matumizi ya tovuti zetu, kitendo cha mtumiaji yeyote (iwe mtandaoni au nje ya mtandao) katika hali yoyote ile, au vinginevyo. Hatutawajibikia uharibifu wowote wa kompyuta, programu, modemu, simu au mali nyingine unaotokana na utumiaji wako wa (au kutoweza kwako kutumia) tovuti zetu. Hatutawajibika ikiwa huwezi kufikia maelezo kupitia tovuti zetu. Baadhi ya nchi haziruhusu kutojumuishwa au vikomo vya baadhi ya dhima na/au dhamana, hivyo baadhi ya vikomo vilivyotajwa hapa juu huenda havitumiki kwako.

Kikomo cha Dhima

Katika hali yoyote ile, BibleProject AU WAFANYAKAZI WAKE, WAKURUGENZI, MAAFISA, WAKALA, WASAMBAZAJI AU WATOA HUDUMA WAKE HAWATAWAJIBIKA KWA NIABA YAKO AU MTU MWINGINE YOYOTE KUHUSIANA NA AU KUTOKANA NA MATUMIZI YA TOVUTI AU MAUDHUI YETU, IKIJUMUISHA, LAKINI SIO TU, KUWAJIBIKIA UHARIBIFU KATIKA MATUKIO MAALUM, USIO WA MOJA KWA MOJA, WA KIPEKEE, AU UNAOSABABISHWA NA HALI FULANI AU UHARIBIFU WOWOTE ULE, IKIJUMUISHA LAKINI SIO TU, KUACHA KUTUMIKA, KUPOTEZA DATA, FAIDA AU NIA NJEMA, KUKATIZWA KWA BIASHARA, AU KOMPYUTA KUACHA KUFANYA KAZI AU KUKUMBWA NA HITILAFU, BILA KUZINGATIA KITENDO CHOCHOTE, IKIJUMUISHA LAKINI SIO TU MKATABA, DHIMA KALI, UTEPETEVU, AU VITENDO VINGINE VISIVYO HALALI, VYOYE KUTOKANA NA AU VINAVYOHUSIANA NA MATUMIZI, KUTOWEZA KUTUMIA, KUTOA NAKALA, AU KUONYESHA MAUDHUI. KIKOMO HIKI KINATUMIKA KATIKA MADAI YOTE IKIWEMO, LAKINI SIO TU, UKIUKAJI WA MKATABA, UKIUKAJI WA DHAMANA, KUHARIBU SIFA, DHIMA KALI, KUWAKILISHWA VISIVYO, DHIMA YA BIDHAA, UKIUKAJI WA SHERIA (IKIJUMUISHA MASHARTI), UTEPETEVU, NA VITENDO VYA ULEGEVU, PAMOJA NA MADAI YA WATU WENGINE.

Pamoja na vipengee vilivyotajwa awali, kikomo cha kiasi jumla cha dhima ambacho wewe au mtu mwingine anaweza kudai BibleProject kitawekwa kuwa kiwango cha juu zaidi cha kiasi chochote ambacho umelipa BibleProject katika miezi 12 iliyopita.

Kufidia

UNAKUBALI KUTUFIDIA, KUFIDIA KAMPUNI ZETU TANZU NA TUNAZOMILIKI, PAMOJA NA WASHIRIKI WAO, WAKURUGENZI, MAAFISA, MAWAKALA, WASHIRIKA NA WAFANYAKAZI, NA KUTOTUHUSISHA NA HASARA, DHIMA, GHARAMA, MALIPO, MADAI, UHARIBIFU, AU SHURUTISHO, IKIJUMUISHA LAKINI SIO TU MALIPO YA WAKILI, KUTOKANA AU KUHUSIANA NA (I) MATUMIZI YAKO YA TOVUTI ZETU KWA NJIA INAYOKIUKA SHERIA NA MASHARTI YETU, (II) UKIUKAJI WAKO WA SHERIA NA MASHARTI YETU, AU (III) UKIUKAJI WOWOTE WA DHIMA NA IDHINI YAKO KATIKA SHERIA NA MASHARTI YETU.

Kubadilishwa kwa Sheria na Masharti haya

BibleProject ina haki ya kubadilisha Sheria na Masharti haya kwa kusasisha toleo hili bila kukujulisha mapema. Tunaweza kubadilisha au kusasisha Sheria na Masharti haya ya Matumizi wakati wowote kwa sababu yoyote, baada ya kukuarifu mapema au bila kufanya hivyo, na mabadiliko hayo ya Sheria na Masharti haya yatachukua nafasi ya na kutumika badala ya Sheria na Masharti ya awali pindi ukurasa huu umechapishwa. Unakubali kuwa endapo kipengee chochote kwenye Sheria na Masharti haya kitapatikana kuwa hakiwezi kutekelezwa, vipengee hivyo vingine kwenye Sheria na Masharti haya vitaendelea kutekelezwa kikamilifu na kipengee hicho husika kitarekebishwa ili kiweze kutekelezwa kadri inavyoruhusiwa kisheria. Unakubali kuzingatia marekebisho yoyote kama hayo. Unashauriwa utembelee ukurasa huu mara kwa mara ili uangalie toleo linalotumika la Sheria na Masharti.

Kusalimisha Haki ya Kuwasilisha Kesi kama Kikundi

Unasalimisha haki yoyote ya kushiriki au kuwasilisha kesi yoyote dhidi ya BibleProject kama kikundi, kuhusiana na madai, mgogoro au utata, na, inapohitajika, unakubali kujiondoa kwenye kesi inayoendelea iliyowasilishwa na kikundi dhidi ya BibleProject.

Makubaliano ya Upatanishi

Kumbuka: Makubaliano haya ya Upatanishi yanatumika tu kwa watumiaji wanaoishi Marekani.

WEWE NA TBP MNAKUBALI KUSALIMISHA HAKI ZOZOTE ZA KUWASILISHA KESI KORTINI AU MBELE YA BARAZA LA MAHAKAMA AU KUSHIRIKI KATIKA KESI KAMA KIKUNDI AU KUHUSISHA WAKILI KUHUSIANA NA MADAI. PIA, HUENDA HAKI ZINGINE AMBAZO UNGEKUWA NAZO IWAPO UNGEKWENDA KORTINI, KAMA VILE KUPATA USHAHIDI, HAZIPATIKANI AU ZIMEWEKEWA VIKWAZO KWENYE UPATANISHI.

Madai au mizozo yoyote inayotokana au inayohusiana na Sheria na Masharti haya pamoja na ufasiri, ukiukaji, ukomeshaji au uhalali wake, uhusiano unaotokana na Sheria na Masharti haya, ikiwemo mizozo kuhusu uhalali, upeo au utekelezaji wa kipengee hiki cha upatanishi (kwa pamoja yanarejelewa kama, "Mizozo Maalum") itatatuliwa kwa njia ya kipekee kupitia ushurutishaji, upatanishi binafsi, badala ya kortini, na itafanyika Portland, Oregon au kwingine ambako wahusika watakubaliana. Upatanishi utafanywa na Shirika la Upatanishi la Marekani ("AAA") kwa mujibu wa sheria na kanuni zake. Sheria za Upatanishi za Serikali inasimamia ufasiri na utekelezaji wa Makubaliano haya ya Upatanishi. Badala yake, unaweza kuwasilisha madai yako kwenye korti maalum za upatanishi, ikiwa madai yako yanastahiki na mradi kesi isalie kwenye korti hiyo na iendeshwe kama kesi baina ya watu binafsi (isiyo ya kikundi, isiyohusisha wawakilishi).

Kabla ya kuwasilisha kesi yoyote ya upatanishi, anayewasilisha atamjulisha mhusika wa pili kuhusu nia yake ya kuwasilisha kesi ya upatanishi kwa kumwandikia notisi angalau siku 60 kabla ya kufanya hivyo. TBP itakutumia notisi hii kupitia barua pepe kwa anwani yako ya barua pepe iliyo kwenye rekodi zetu na sharti utoe notisi hio kupitia barua pepe kwa webmaster@jointhebibleproject.com. Wakati wa kipindi cha notisi cha siku 60, wahusika watajitahidi kusuluhisha Mizozo yoyote Maalum kwa njia ya amani. Wahusika wakishindwa kusuluhisha mzozo na muda wa notisi ukikwisha, mhusika yoyote anaweza kuwasilisha kesi ya upatanishi.

Mpatanishi ana uwezo wa kutoa uamuzi wowote unaoweza kuchukuliwa kortini chini ya sheria au kwa usawa na uamuzi wake/wao utatekelezwa na utakuwa wa kushurutisha kwa kila mhusika. Rufaa kuhusu uamuzi uliotolewa na mpatanishi inaweza kukatwa katika korti yoyote inayostahiki. Pamoja na wajibu uliotajwa awali wa kusuluhisha mizozo, kila mhusika atakuwa na haki ya kuwasilisha ombi la kupata agizo linalomlinda au uamuzi mwingine sawa wakati wowote, kwenye korti yoyote inayostahiki. Mpatanishi atatumia sheria husika pamoja na vipengee vya Sheria na Masharti haya na asipofanya hivi itachukuliwa kuwa anatumia mamlaka vibaya na hiki kitakuwa kigezo cha kupinga uamuzi wake. Wewe na TBP hamruhusiwi kusuluhisha Mzozo wowote Maalum kama kesi ya kikundi, ya uwakilishi au inayohusisha wakili wa kibinafsi na mpatanishi/wapatanishi hawaruhusiwi kusikiliza kesi ya kikundi, ya uwakilishi au inayohusisha wakili wa kibinafsi. Iwapo kipengee chochote cha upatanishi kwenye makubaliano kitapatikana kuwa si halali au hakiwezi kutekelezwa, vifungu hivyo vingine vya upatanishi vitaendelea kuwa halali, vya kushurutisha na kutekelezwa kikamilifu (lakini katika hali yoyote ile, hakutakuwepo na kesi ya kikundi, uwakilishi au inayohusisha wakili wa kibinafsi). Sheria na Masharti haya ya Matumizi na shughuli husika zitasimamiwa na zitatumika kwa mujibu wa Sheria za Upatanishi za Serikali, 9 U.S.C. sehemu ya 1-16 (FAA) na, inapohitajika, sheria za Jimbo la Oregon.

 

By using this website, I acknowledge that I am 16 years of age or older, and I agree to the Terms and Conditions and Privacy Policy.
Under 16?
Accept
For advanced bible reading tools:
Login  or  Join
Which language would you like?