Back

Sera ya Faragha

BibleProject

Ilifanyiwa Mapitio Agosti 2019

Utangulizi

BibleProject inaheshimu fargha yako na imejitolea kulinda taarifa zako muhimu. Sera hii ya Faragha ("Sera ya Faragha") ni makubaliano kati yako na BibleProject na washirika wake, kampuni mama, na kampuni tanzu (ambazo kwa pamoja zinaitwa "BibleProject"," sisi ", "yetu ", au"sisi ") unapofungua na kutumia tovuti zetu, ikiwa ni pamoja na thebibleproject.com, mitandao ya jamii, programu za simu na huduma (zinazorejelewa kwa pamoja kama, "Tovuti"), na inasimamiwa na ni sehemu ya  Masharti ya Matumizi ya BibleProject.

Taarifa za Kibinafsi

Kama linavyotumika katika Sera hii ya Faragha, "Taarifa za Kibinafsi" ina maana ya taarifa zinazomtambulisha mtu binafsi (k.m. jina, anwani, nambari ya simu, barua pepe, jina la mtumiaji, au nambari ya kadi ya benki), au taarifa kuhusu mtu huyo zinazohusiana moja kwa moja na taarifa zinazoweza kumtambulisha mtu binafsi. Taarifa za Kibinafsi si pamoja na (a) taarifa za jumla, kwa maana ya data ya matumizi yako ya Tovuti yetu au kuhusu kundi au aina ya huduma au watumiaji, ambayo ina taarifa za kibinafsi au Taarifa nyingine za Kibinafsi zimechukuliwa (b) taarifa za kibinafsi ambazo haziwezi kuhusishwa na mtu binafsi kwa urahisi.

Sera hii ya Faragha inaelezea utaratibu tunaofuata katika kukusanya, kutumia, kuhifadhi, kulinda, na kufichua Taarifa zako za Kibinafsi, pamoja na mawasiliano yako na BibleProject kupitia kwa njia ya simu, barua pepe au hata kutembelea ofisi zetu.

Tafadhali soma sera hii kwa umakini mkubwa ili uelewe sera na taratibu zetu kuhusiana na taarifa zako na namna tunavyoisimamia.

Ridhaa

Kwa kutembela Tovuti hii, kuunda wasifu wa mtumiaji kwenye Tovuti hii, kutembelea studio yetu, au kuwasilisha Taarifa zako za Kibinafsi kwa BibleProject, unakubaliana na Sera hii ya Faragha na ukusanyaji na matumizi ya Taarifa zako za Kibinafsi kama ilivyoainishwa hapa chini. Tutachukua hatua za kukuarifu na kuthibitisha kwamba unakubaliana katika hatua mbalimbali za kukusanya Taarifa zako za Kibinafsi kutoka kwako. Kama hukubaliani na sera na taratibu zetu, huenda usiweze kufikia au kufaidika kutoka kwa sehemu fulani kwenye Tovuti hii.

Wigo

Tafadhali fahamu kwamba Sera hii ya Faragha inahusu taarifa tunazokusanya:

 • unapotembelea Tovuti hii.

 • unapotembelea studio yetu.

 • unapotupatia taarifa zako.

 • unapounda au kutumia wasifu wa mtumiaji.

 • tunapowasiliana nawe kwa barua pepe na njia nyingine.

 • kupitia washirika wengine tunaoshirikiana nao kutoa huduma zetu.

 • kwa njia nyingine katika kipindi chote utakachotumia huduma zetu.

Sera hii haitumiki kwenye taarifa zako zinazokusanywa kwa njia nyingine yoyote, ikiwa ni pamoja na programu za simu, maudhui, au tovuti ambazo hazimilikiwi na BibleProject.

Misingi ya Kisheria

Tutakusanya Taarifa zako za Kibinafsi (a) zinapohitajika tu, kwa idhini yako au (b) ikiwa tuna sababu za msingi za kufanya hivyo. Ikiwa tutakusanya au kutumia Taarifa zako za Kibinafsi kwa idhini yako, pia tutakufahamisha kuhusu mabadiliko yoyote na kukuomba utoe idhini nyingine kama inavyotakiwa.

Faragha ya Watoto

BibleProject inatambua umuhimu wa kutoa ulinzi zaidi wa faragha kuhusu Taarifa za Kibinafsi za Watoto. Hatukusanyi Taarifa zozote za Kibinafsi za Watoto walio chini ya umri wa miaka 16 kwa kujua bila kupata ridhaa ya mzazi au mlezi wa mtoto. Ikiwa mtoto aliye chini ya miaka 16 angependa kujisajili kwenye Tovuti hii, BibleProject itamtaka mzazi au mlezi wa mtoto kutoa ridhaa ya kusajiliwa kupitia mchakato wetu wa barua pepe ya kuthibitisha kabla ya kukubali usajili wa mtoto. BibleProject isipopokea ridhaa ya mzazi au mlezi ndani ya saa 24 baada ya mtoto kutuma ombi la kujisajili, tutafuta Taarifa zozote za Kibinafsi ambazo huenda mtoto huyo alitupatia wakati wa kutuma ombi lake la kusajiliwa. Ikiwa umri wako ni chini ya miaka 16 na mzazi au mlezi wako hajakamilisha mchakato wa Tovuti yetu wa kusajiliwa na ridhaa, BibleProject inakupa maelekezo ya kutotumia Tovuti hii, kununua au kutoa michango kupitia kwenye Tovuti hii, kutumia vipengele vya kuwasiliana au kutoa maoni vya Tovuti hii, au kutoa Taarifa zozote za Kibinafsi kwa BibleProject.

BibleProject ni shirika lisilo la faida kwa mujibu wa 501(c)(3) kwa hiyo haisimamiwi na Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni. Hata hivyo, BibleProject inathamini sana faragha ya watoto ambao wanaweza kufaidi kutokana na maudhui yetu. Masharti yote ya Sera hii ya Faragha yanatumika kwa watumiaji wote wa Tovuti hii, ikiwa ni pamoja na watoto. Watoto wanaotembelea tovuti wanafaa kushauriana na wazazi au walezi wao daima kabla ya kuweka taarifa zao kwenye tovuti au programu yoyote ya simu, na tunahimiza familia kujadili miongozo ya kaya zao kuhusu kuweka Taarifa za Kibinafsi mtandaoni.

Ikiwa unaamni kwamba huenda BibleProject ina taarifa kutoka au kuhusu mtoto aliye chini ya umri wa miaka 16 bila ridhaa ya mzazi au mlezi, au ikiwa ungependa kupitia au kutuma maombi ya kufuta Taarifa Binafsi za mtoto wako ambazo ziko kwenye BibleProject, tafadhali wasiliana nasi kupitia webmaster@jointhebibleproject.comau utupigie simu bila malipo kwenye (855) 700-9109.

Jinsi Tunavyokusanya na Kutumia Taarifa zako za Kibinafsi

Unapotembelea Tovuti au studio yetu, tunakusanya Taarifa fulani za Kibinafsi kutoka kwako. Tunakusanya taarifa hizi:

 • Moja kwa moja kutoka kwako unapotupatia.

 • Kiotomatiki unapoperuzi Tovuti.

 • Kutoka kwa washirika wengine, ikiwa ni pamoja na tovuti nyingine.

Tafadhali kumbuka kwamba unaweza kufikia tu baadhi ya ofa, huduma, na sehemu za Tovuti yetu ikiwa umejisajili. Uko huru kupunguza taarifa unazotupatia hadi kwa chache ambazo ni muhimu katika kupata huduma zetu, na unaweza kuwasiliana na BibleProjectwakati wowote ili kuhariri taarifa tulizonazo kukuhusu. Hata hivyo, tafadhali kumbuka kwamba iwapo utakataa kutupatia Taarifa zako za Kibinafsi, au ubatilishe ridhaa yako, bila shaka hututaweza kuwasiliana na wewe au kukupa huduma zetu.

Taarifa Unazotupatia.

Tunakusanya Taarifa za Kibinafsi moja kwa moja kutoka kwako kwa ridhaa yako unapotembelea studio yetu au kuwasiliana nasi kwenye Tovuti yetu. Taarifa za Kibinafsi unazotupatia zinaweza kuwa pamoja na:

 • Maelezo ya Mawasiliano- Tunachukua jina lako, nambari ya simu, anwani ya barua pepe na eneo unakoishi unapojaza na kuwasilisha fomu za kielektroniki kwenye Tovuti yetu. Tunatumia taarifa hizi kukusajili kwenye Tovuti yetu, kukutumia majarida, pamoja na kukupa taarifa, bidhaa na huduma zetu. Pia tunaweza kukuomba taarifa zako unaporipoti hitilafu kwenye Tovuti yetu.

 • Maudhui ya Mtumiaji- Tovuti yetu inaweza kujumuisha vipengele vinavyokuruhusu kuchapisha maoni, picha, au maudhui mengine, kwa mujibu wa Sheria zetu za Matumizi. Uamuzi ni wako iwapo ungetaka kutumia vipengele hivi na taarifa zozote au maudhui unayochapisha yanatolewa kwa hiari yako. Tunaweza kuweka rekodi na nakala za barua zako (ikiwa ni pamoja na anwani za barua pepe), ikiwa utachapisha Maudhui ya Mtumiaji au kuwasiliana nasi.

 • Taarifa za Malipo- Tunapokea malipo na michango kupitia kwenye Tovut yetu. Tunatumia kampuni nyingine ya kuchakata malipo, Stripe, kushughulikia miamala yote. Unapofanya malipo mtandaoni, Tovuti itakuelekeza kwenye ukurasa wa Stripe wa Malipo ya BibleProject. Stripe ni kampuni inayotoa huduma za kuchataka malipo ya mtandaoni zinazokidhi vigezo vya PCI. BibleProject haikusanyi, kuchakata au kuhifadhi taarifa za malipo, lakini tunaweza kuweka rekodi za miamala unayofanya kwenye Tovuti yetu na kulipia oda zako. Tukiwa na tatizo lolote la kuchakata oda, tutatumia maelezo yako ya mawasiliano kuwasiliana nawe.

 • Taarifa za Ana kwa Ana- Unapotembelea studio ya BibleProject, tutakuomba ujaze fomu ya wageni na tutanasa picha yako kwa kutumia kamera za jengo unapoingia na kutoka kwenye jengo letu au eneo la studio. Tunakusanya taarifa hizi kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi na wageni wetu. Pia, kulingana na madhumuni ya kututembelea, tunaweza kukuomba ujaze fomu za ziada. Tutakujulisha madhumuni ya fomu hizi wakati wa kuzichukua.

Taarifa Tunazokusanya Kupitia Teknolojia za Kukusanya Data Kiotomatiki.

Unapokuwa ukiperuzi na kutumia Tovuti yetu, tunaweza kutumia teknolojia za kukusanya data kiotomatiki kama vile vidakuzi vya kuchambua data kukusanya taarifa fulani kuhusu kifaa chako, tovuti na ruwaza za mwenendo wako wa kuperuzi. Tunakusanya taarifa hizi ili kufikia maslahi yetu halali ya kudumisha na kuboresha Tovuti pamoja na kutathmini mafanikio ya yetu ya kuwafikia watu na  juhudi zetu za mauzo. Taarifa tunazokusanya kupitia teknolojia hizi za kukusanya data kiotomatiki ni pamoja na:

 • Faili za Kumbukumbu- Tunakusanya taarifa zisizokuwa na majina na za kiufundi kutoka kwenye kompyuta yako, ikiwa ni pamoja, data ya shughuli, data ya eneo, kumbukumbu, na data nyingine ya mawasiliano na nyenzo unazofungua na kutumia kwenye Tovuti yetu. Pia tunakusanya taarifa kuhusu kompyuta yako, kifaa, na muunganisho wako wa intaneti, ikiwa ni pamoja na anwani ya IP yako, mfumo wa uendeshaji, aina ya kifaa, na aina ya kivinjari. Tunafanya taarifa hii isiwe na jina ili isikutambulishe na ili isitumike kufuatilia mwenendo wako mtandaoni. Pia tunatumia taarifa hii kukadiria ukubwa wa hadhira yetu na ruwaza za matumizi, kuhifadhi taarifa za vitu unavyopenda, kubadilisha mipangilio ili kuboresha huduma unazopata, kuharakisha majibu ya utafutaji pamoja na kukutambua unaporudi kwenye Tovuti yetu. Uchambuzi huu unatusaidia kuboresha Tovuti yetu na kutoa huduma bora na mahususi kwa mahitaji yako

 • Barua pepe- Barua pepe zetu zimepachikwa msimbo wa kufuatilia ili kufuatilia mlengwa anapopokea na kufungua barua pepe na anapotumia kiungo kilicho kwenye barua pepe kutembelea Tovuti yetu.

 • Vidakuzi- Kama ilivyo kwa tovuti nyingi za kibiashara, tunatumia vidakuzi kufuatilia matumizi ya Tovuti yetu. Tafadhali soma Sera yetu ya Vidakuzi kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyotumia vidakuzi.

Taarifa tunazokusanya kiotomatiki ni pamoja na Taarifa za Kibinafsi, au tunaweza kuweka taarifa hizo au kuzihusisha na Taarifa za Kibinafsi tunazokusanya kwa njia nyingine au tunazopokea kutoka kwa washirika wengine.Taarifa hizi zinaweza kuwekwa pamoja kwenye muhtasari wa taarifa ya wanaotembelea tovuti na wingi wa shughuli. Ikiwa hungependa BibleProject ikusanye na kutumia data yako ya kiufundi na bila kukutaja jina kama ilivyoelezewa katika aya hii, acha kututmia Tovuti hii mara moja, au wasiliana nasi kama ilivyoelezwa kwenye "Kudhibiti Taarifa zako za Kibinafsi" hapa chini.

Taarifa Tunazokusanya kutoka Kwenye Tovuti Nyingine

BibleProject huwafuatilia watumiaji kadhaa wanaotembelea Tovuti yetu kutoka kwenye mitandao ya jamii  (k.m., Facebook, YouTube au Twitter) kutimiza maslahi yetu halali ya kupima ufanisi wa matangazo yetu kwenye mitandao ya jamii na machapisho. Ukitembelea Tovuti yetu kutoka kwenye tovuti za mitandao ya jamii, au ikiwa utakubali kuhusisha akaunti yako nasi kwa tovuti ya mitandao ya jamii, pia tunaweza kupokea Taarifa zako za Kibinafsi kutoka kwenye tovuti ya mtandao huo wa jamii. Tafadhali kumbuka kwamba tovuti za mitandao ya jamii ambapo huenda tukapata Taarifa zako za Kibinafsi hazidhibitiwi wala kusimamiwa na BP. Maswali yoyote yanayohusu jinsi tovuti ya mtandao wa jamii inavyokusanya au kuchakata Taarifa zako za Kibinafsi yanafaa kuelekezwa kwa mtoa huduma ya mtandao husika wa jamii. Tunaweza kuweka taarifa hizi pamoja na taarifa tunazokusanya moja kwa moja kutoka kwako.

Njia Nyingine Tunazotumia Taarifa Zako

Pia tunaweza kutumia Taarifa za Kibinafsi tunazokusanya kutoka kwako au zako:

 • Kuunda na kuboresha bidhaa na huduma zetu.

 • Kukufikishia Tovuti yetu na maudhui yake.

 • Kukupa taarifa, bidhaa, au huduma unazoomba kutoka kwetu.

 • Kutimiza madhumuni mengine yoyote ambayo unayakusudia kutumia.

 • Kutekeleza wajibu wetu na kutumia haki zetu zinazotokana na mikataba tuliyoingia kati yako na sisi, ikiwa ni pamoja na kufanya malipo na kukusanya.

 • Kukujulisha kuhusu mabadiliko kwenye Tovuti au bidhaa au huduma zozote tunazotoa kupitia tovuti hii.

 • Kukuruhusu kutumia vipengele vya mawasiliano vinavyopatikana kwenye Tovuti yetu.

 • Kulinda faragha yako na kutekeleza hii Sera ya Faragha.

 • Kulinda haki na hakimiliki zetu.

 • Ikiwa tunaamini kwamba kuna haja ya kutambua, kuwasiliana au kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaokusababishia kadhia, BibleProject, au watu wengine, au ili kukidhi matakwa ya kisheria, masharti, au mchakato wa kisheria au agizo la mahakama.

 • Katika njia nyingine yoyote tutakayofafanua utakapotoa taarifa hii.

 • Kwa madhumuni mengine yoyote kwa ridhaa yako.

BibleProject inaweza kutumia vidakuzi au wavuti wa shirika lingine kukusanya na kuchambua Taarifa zako za Kibinafsi au shughuli zako kwenye Tovuti yetu (k.m., kubonyeza taarifa za mtiririko, aina ya kivinjari, saa na dakika, mada uliyobonyeza au kutelezesha) ili zitusaidie kuanisha matangazo ambayo yana tija kwako. Ikiwa unapendelea BibleProject isitumie taarifa kulingana na mwenendo wako mtandaoni ili kukupa maudhui na matangazo mahususi kwa ajili yako, unaweza kujiondoa kwenye matangazo ya mwenendo wako wa matumizi ya mtandao kwa kufuata maelekezo yafutayo ya Kujiondoa Kwenye Mawasiliano.

Tunaweza kuunganisha taarifa zako tunazokusanya kupitia kwa Huduma na taarifa nyingine kukuhusu tunazopokea kutoka kwa vyanzo vya mashirika mengine. Kwa mfano bila ukomo, tunaweza kutumia mabadiliko ya eneo la makazi au huduma nyingine zilizoorodheshwa kuhakikisha kwamba rekodi zetu za akaunti yako ni sahihi.

Kufichua Taarifa Zako

BibleProject haitauza Taarifa zako za Kibinafsi kwa shirika lingine lolote. Tunaweza kufichua Taarifa za Kibinafsi tunazokusanya au unazotupatia kama Sera hii ya Faragha inavyofafanua.

 • Kwa kampuni tanzu na washirika wetu.

 • Kwa wazabuni, wachakataji wa malipo, watoa huduma, na mashirika mengine tunayotumia kuendesha biashara yetu.

 • Kwa mnunuzi au shirika lingine linalochukua uongozi iwapo biashara yetu itaingia ubia na shirika lingine, kuuza kampuni tanzu, kubadilisha mpangilio, kuratibu upya biashara yetu, kufunga, au kuuza au kuhawalisha baadhi ya mali za  BibleProject, ama kutokana na changamoto au kama sehemu ya kufilisika, kuuzwa, au michakato mingine kama hiyo, ambayo itasababisha Taarifa zako za Kibinafsi zinazoshikiliwa na BibleProject kuhusu watumiaji wa Tovuti yetu kuwa miongoni mwa mali itakayohamishwa.

 • Kwa washirika wetu wa kutangaza na uchambuzi wa data kama Google Analytics. Makampuni haya mengine yanatumia Sera yao ya Faragha kukusanya, kutumia na kufichua taarifa zako. Mashirika haya mengine yanaweza kuweka taarifa zako na za wateja wengine pamoja kwa ajili ya kufanya tafiti hizi na/au uchambuzi . Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea Google Analytics Opt-out Browser Add-On.

 • Ili kutimiza madhumuni ya taarifa unazotupatia. Kwa mfano, ukitupatia anwani ya barua pepe ili utumie kipengele cha Tovuti yetu cha"kumtumia rafiki barua pepe", tutatuma maudhui yaliyo kwenye barua pepe hiyo na anwani yako ya barua pepe kwa wapokeaji.

 • Kwa ajili ya madhumuni mengine yoyote tunayobainisha unapotoa taarifa zako.

 • Kwa ridhaa yako.

Pia tunweza kufichua Taarifa zako za Kibinafsi:

 • Katika kutekeleza agizo lolote la mahakama, sheria, au mchakato wa kisheria, ikiwa ni pamoja na kujibu barua za taasisi ya serikali au ombi la udhibiti.

 • Kutekeleza au kuzingatia Sheria zetu za Matumizi na mikataba mingine, ikiwa ni pamoja na madhumuni ya malipo na kukusanya.

 • Ikiwa tunaamini kwamba ni muhimu au sahihi ili kulinda haki, mali, au usalama wa BibleProject, wateja wetu au watu wengine.

Taarifa Jumla

Tunaweza kutuma taarifa jumla au kuondoa utambulisho wa taarifa bila kikwazo. Taarifa tunayotoa haitakutambulisha wewe binafsi. Hata hivyo, inawezekana kwamba mashirika mengine yanaweza kuunganisha taarifa hii ya jumla pamoja na data yako nyingine waliyonayo, au wanayopokea kutoka kwa mashirika mengine, kwa namna inayowaruhusu kukutambua wewe binafsi.

Kusimamia Taarifa zako za Kibinafsi

Ikiwa wewe ni raia wa Umoja wa Ulaya, una haki nyingine za ziada kuhusu Taarifa zako za Kibinafsi. Una haki ya kutumia haki hizi, kuuliza maswali, au kupata taarifa za ziada kuhusu matumizi ya Taarifa zako za Kibinafsi kwa kuwasiliana nasi kwa kupiga simu kwa (855) 700-9109 bila malipo au kutuandikia barua pepe kupitia webmaster@jointhebibleproject.com.


Una haki ya...

Hii ina maana gani kwako

Unachoweza kufanya

Fahamu kuhusu jinsi Taarifa zako za Kibinafsi zitakavyochakatwa.

Tutakujulisha kupitia kwa Sera hii ya Faragha kuhusu jinsi tutakavyotumia Taarifa zako za Kibinafsi, kwa madhumuni gani na nani mwingine anaweza kuzifikia.

Tafadhali soma Sera hii ya Faragha kwa makini na uwasiliane nasi iwapo una maswali yoyote.

Fikia Taarifa zako za Kibinafsi.

Baada ya kupokea maombi, tutakupatia uwezo wa kufikia Taarifa zako za Kibinafsi tulizonazo kukuhusu, yaani aina ya taarifa zako tulizonazo, tunavyozikusanya, kuzitumia, na nani anaweza kuzifikia.

Unaweza kutuma maombi ya kupewa nakala ya Taarifa za Kibinafsi tunazochakata kukuhusu. Katika mazingira fulani, sheria inaweza kututaka au kutukubalia kukunyima baadhi au data yote unayoitisha.

Kuzuia uchakataji wa Taarifa zako za Kibinafsi katika mazingira fulani.

Katika mazingira fulani na kwa kiasi kinachokubalika kisheria, tutazuia uchakataji wa Taarifa zako za Kibinafsi.

Unaweza kutuma ombi la kuzuia uchakataji wa Taarifa zako za Kibinafsi ikiwa (i) Taarifa hizo za Kibinafsi si sahihi, (ii) uchakataji unakiuka sheria, (iii) hatuhitaji Taarifa hizo za Kibinafsi, au (iv) unatumia haki yako ya kupinga uchakataji (soma hapa chini).

Kusahihisha Taarifa za Kibinafsi tulizonazo kukuhusu.

Tunatakiwa kuchukua hatua za kulinda usahihi wa Taarifa za Kibinafsi tunazochakata.

Ukigundua kwamba Taarifa zako za Kibinafsi tulizonazo sio sahihi au ukibadilisha Taarifa zako za Kibinafsi (k.m. jina au eneo unakoishi), tafadhali tujulishe na tutasasisha rekodi zetu.

Kuhamishika kwa data.

Katika  mazingira fulani, tutatakiwa kuhamisha Taarifa zako za Kibinafsi kwenye shirika lingine kufuatia ombi lako.

Una haki ya kutuma maombi ya kuhamisha Taarifa za Kibinafsi tulizonazo kukuhusu kwa shirika lingine katika muundo wa kawaida unaoweza kusomwa na kompyuta.

Kufuta Taarifa zako za Kibinafsi (yaani "haki ya kusahauliwa").

Katika mazingira fulani na tunapotakiwa kufanya hivyo kisheria, ni lazima tufute Taarifa za Kibinafsi tulizonazo kukuhusu kwa ombi lako. Haki hii inaweza kubatilishwa. Kuna hali ambazo hatutakuwa na wajibu wa kutekeleza ombi lako.

Una haki ya kutuma maombi kwetu kufuta Taarifa zako za Kibinafsi. Ukitoa ombi hili, tutahitaji kusawasisha matakwa fulani ya kisheria, mkataba wetu na wewe na maslahi ya biashara dhidi ya haki yako ya kutoa ombi la kufuta Taarifa muhimu za Kibinafsi.

Kukataa uchakataji fulani wa Taarifa zako za Kibinafsi.

Ukikataa uchakataji wa Taarifa zako za Kibinafsi, tutazingatia sheria, mkataba wetu na wewe na maslahi ya biashara pamoja na wajibu wetu katika kufanya maamuzi dhidi ya haki yako ya kukataa uchakataji huu.

Katika mazingira fulani unaweza kukataa uchakataji wa Taarifa zako za Kibinafsi. Pia unaweza kukataa Taarifa zako za Kibinafsi zisitumike kwa madhumuni ya moja kwa moja ya kibiashara.

Taarifa zako zisiathirike na maamuzi yanayotokana na uchakataji otomatiki (yaani, maamuzi ya programu za kompyuta yanayokuathiri bila mwanadamu kuhusika).

Katika mazingira fulani, ni lazima tukupatie haki ya kupinga maamuzi tunayofanya kwa uchakataji otomatiki. Sambamba na hilo, tunatakiwa kuweka kumbukumbu za uchakataji otomatiki na kutoa taarifa kuhusu utaratibu unaofuatwa katika kufanya maamuzi haya.

Unaweza kupinga uamuzi unaofanywa na uchakataji otomatiki ikiwa uamuzi huo ulifanywa na programu ya kompyuta bila mwanadamu kuhusika.

Tutatekeleza ombi lako la kutumia yoyote kati ya haki hizi ndani ya siku 30 baada ya kupokea ombi lako. Pia una haki ya kusahihisha makosa yoyote yaliyo kwenye taarifa hizo. Tafadhali kumbuka kwamba BibleProject, kisheria inatakiwa ithibitishe utambulisho wako kabla ya kutekeleza ombi lako, katika kufanya hivyo inaweza kukuitisha Taarifa zaidi za Kibinafsi.

Tuandikie barua kwa anwani BibleProject 501 SE 14th Avenue Portland, OR 97214

Haki za Faragha za California

Kwa sababu BibleProject haijaundwa au kuendeshwa ili kujipatia faida au manufaa ya kifedha kwa wanahisa wake au wamiliki wengine, tuna ruhusa ya kutofuata Sheria ya California ya Faragha ya Mteja (maarufu kama "CCPA"; Ca. Sehemu za Sheria za Umma za 1798.100 - 1798.199). Hata hivyo, baadhi ya mikataba yetu na watoa huduma na mashirika mengine inatutaka kufuata sheria ya CCPA. Watumiaji wa Tovuti yetu ambao ni wakazi wa jimbo la California wanaweza kuwa na haki fulani zinazohusu Taarifa zao za Kibinafsi, kama vile haki ya (a) kupata taarifa zinazoelezea aina ya Taarifa zako za Kibinafsi tulizokusanya, na iwapo taarifa hizi ziliuziwa mashirika mengine; (b) kupokea orodha ya aina za washirika wengine ambao tumeshiriki  Taarifa zako za Kibinafsi nao; (c) ikiwa tunauza Taarifa zako za Kibinafsi, tupe maagizo ya kutouza Taarifa zako za Kibinafsi kwa washirika wengine; na (d) kupokea huduma kwa usawa bila kujali kama umetumia haki zako za faragha.

Isitoshe, Sehemu ya 1798.83-1798.84 ya Sheria za Umma za California inawapa wakazi wake haki ya kupewa stakabadhi inayoonesha aina za Taarifa za Kibinafsi tunazotuma kwa wabia na/au washirika wengine kwa ajili ya matangazo ya kibiashara, na kutoa maelezo ya mawasiliano ya wabia hao na/au washirika wengine.

Ikiwa wewe ni mkazi wa California na ungependa kupata nakala ya Sera hii ya Faragha au kutumia haki zako zinazopatikana chini ya sheria zinazohusika za California, tafadhali tupigie simu kupitia (855) 700-9109 bila malipo au ututumie barua pepe kwenye webmaster@jointhebibleproject.com ikiwa na kichwa "Ombi la Maelezo ya Faragha California."

Kujiondoa Kwenye Mawasiliano

Tungependa kuwasiliana na wewe ikiwa tu ungependa kuwasiliana nasi. Unaweza kubadilisha au kuweka ukomo kwenye idadi ya ujumbe ambao unapokea kutoka kwa BibleProject kwa kubonyeza kiungo cha  "jiondoe" kilicho katika sehemu ya chini ya barua pepe zozote kutoka kwetu. Pia unaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja kwenye (855) 700-9109 bila malipo au utuandikie barua pepe kwenye webmaster@jointhebibleproject.com. Tafadhali hakikisha kwamba unajumuisha jina lako kamili, anwani ya barua pepe, anwani ya posta, na ubainishe taarifa ambazo unataka kupokea. Ukipenda, unaweza kutumia mojawapo ya kauli zifuatazo kutuandikia ujumbe:

 • Singependa kupokea barua pepe zenye matangazo, kama vile taarifa za bidhaa na huduma, ofa maalumu, au matukio ya baadaye.

Singependa kupokea matangazo ya barua pepe moja kwa moja, kama vile ratiba za vipindi na barua pepe kuhusu bidhaa na huduma, ofa maalumu, au matukio ya baadaye.

Onyo la Do Not Track

Do Not Track ni mapendeleo ya faragha ambayo watumiaji wanaweza kuweka kwenye vivinjari vyao. Mtumiaji anapowasha onyo la Do Not Track, kivinjari hutuma ujumbe kwa tovuti kuziambia zisimfuatilie mtumiaji. Kwa maelezo kuhusu Do Not Track, tembelea www.allaboutdnt.org. Kwa sasa, tovuti ya thebibleproject.com haifanyii kazi mipangilio ya kivinjari au onyo la Do Not Track. Isitoshe, tunaweza kutumia teknolojia nyingine ya kawaida kwenye intaneti kufuatilia wanaotembelea tovuti zetu. Zana hizi zinaweza kutumiwa na washirika wengine kukusanya taarifa kukuhusu na shughuli zako mtandaoni, hata kama umewasha onyo la Do Not Track.

Sheria za Marekani za Faragha

Tovuti hii inamilikiwa na inaendeshwa nchini Marekani. Ukitembelea Tovuti hii ukiwa nje ya Marekani, taarifa zako zote tunazokusanya zitahamishiwa kwenye seva zilizoko Marekani. Sheria za faragha za Marekani huenda hazitalinda faragha yako kama ambavyo sheria za nchi yako zinavyokulinda. Kwa kuturuhusu kukusanya Taarifa za Kibinafsi kukuhusu, unatoa ridhaa ya Taarifa zako za Kibinafsi kuhamishwa na kuchakatwa kama ilivyoainishwa katika Sera hii ya Faragha.

Usalama wa Data

Tumeweka mikakati tunayoweza kugharamia mtandaoni na nje ya mtandao ili kulinda Taarifa zako za Kibinafsi dhidi ya kupotea na kudukuliwa, kutumiwa, kubadilishwa, na kuchapishwa. Tumeweka mikakati pevu ya kulinda nyaraka na data yako ya kielektroniki ili kulinda Taarifa zako za Kibinafsi ambazo hazijulikani na umma. Mikakati hii ni pamoja na kuweka ukomo wa Taarifa zako za Kibinafsi tunazohifadhi kuwa Maelezo ya Mawasiliano, na kutumia teknolojia ya kusimba data. Taarifa za malipo na fedha zinahifadhiwa kwenye seva ya mtoa huduma anayezingatia Viwango vya Kulinda Data vya Sekta ya Malipo ya Kadi (Payment Card Industry Data Security Standard). Taarifa zingine zote za Kibinafsi hutumwa kwa mtoa huduma anayekidhi Vigezo vya Usalama vya Kimataifa kupitia mpango salama ili aihifadhi na kuitunza. Huwa tunaweka teknolojia mpya na kuifanyia majaribio ili kuboresha ulinzi wa taarifa zako na kuhakikisha usalama wa taarifa hizo.

Pia una wajibu katika kuhakikisha usalama na ulinzi wa taarifa zako. Tukikupa (au ukichagua) nenosiri la kuingia sehemu fulani za Tovuti yetu, una wajibu wa kulinda nenosiri hilo. Tunakuhimiza usimpe mtu yeyote nenosiri lako. Pia kumbuka kuondoka kwenye akaunti yako na kufunga dirisha la kivinjari chako ukimaliza kutembelea tovuti yetu. Kufanya hivi kutasaidia kuhakikisha kwamba watu wengine hawawezi kuingia katika akaunti yako, hususan kama unatumia kompyuta yako na mtu mwingine au unatumia kompyuta katika eneo la umma. Watumiaji wote wa intaneti wanatakiwa kuwa makini wanapotumia au kutoa Taarifa zao za Kibinafsi. Maudhui ya Mtumiaji na taarifa nyingine unazoweka katika maeneo ya umma zinaweza kuonwa na mtumiaji yeyote wa Tovuti hii.

Kwa bahati mbaya, hakuna hakikisho la usalama wa taarifa zinazotumwa kwenye intaneti. Ingawa tunafanya kila juhudi kulinda Taarifa zako za Kibinafsi, hatuwezi kukuhakikishia usalama kamilifu wa Taarifa zako za Kibinafsi zinazotumwa kwenye tovuti yetu na kwamba wadukuzi hawawezi kupenya kwenye hatua zetu za usalama au kutumia Taarifa zako za Kibinafsi kwa malengo ambayo hazikukusudiwa. Unawajibikia hatari ya uhamisho wowote wa Taarifa za Kibinafsi. Hatuna wajibu wowote iwapo mipangilio yoyote ya faragha au mikakati ya usalama ya Tovuti yetu itahitilafiwa. Tafadhali tembelea tovuti ya Tume ya Biashara ya Serikali kwa maelezo kuhusu jinsi ya kujilinda dhidi ya wizi wa utambulisho.

Tovuti za Washirika Wengine na Matangazo

Sera hii ya Faragha inatumika kwa taarifa zinazokusanywa na BibleProject tu. Tunaweza kuweka viungo vya tovuti za mashirika mengine kwenye Tovuti yetu kama huduma za watumiaji wetu, lakini hatuna uwezo wa kudhibiti, na hatuna wajibu wa kusimamia faragha na taratibu za ukusanyaji, matumizi, na ufichuzi wa data unaofanyika kwenye tovuti za mashirika mengine. Unapobofya kwenye viungo hivi vinavyokuelekeza kwenye tovuti za nje, utakuwa chini ya sera na taratibu zao za faragha wala si zetu. Tunakuhimiza usome na uelewe sera za faragha za tovuti hizo kabla ya kuwapa taarifa zozote.

Masharti ya Matumizi

Masharti ya Matumizi ya Tovuti hii yanasimamia masuala yote ambayo hayajatajwa kwenye Sera hii ya Faragha. Tunakuhimiza kujizoeza Masharti yetu ya Matumizi.

Mabadiliko ya Sera Yetu ya Faragha

Tunaweza kubadilisha Sera hii ya Faragha mara kwa mara ili kuhakikisha usahihi wake. Tukifanya mabadiliko yoyote, sera mpya itachapishwa kwenye ukurasa huu. Kwa kuendelea kutumia Tovuti na yetu au huduma nyingine baada ya kuchapishwa kwa mabadiliko ya Sera ya Faragha ina maana kwamba umekubali mabadiliko haya. Katika hali fulani, tunaweza kujaribu kuwasiliana na wewe kwa kutumia maelezo ya mawasiliano uliyotupatia, ili kukupatia chaguo kuhusu kutumia taarifa zako kwa njia ambayo ni tofauti na ile uliyoambiwa wakati wa kuchukua taarifa zako. Tafadhali tembelea tovuti yetu mara kwa mara, hasa kabla ya kutupatia Taarifa zako za Kibinafsi, ili kujua wigo wa sasa wa sera yetu.

Matumizi Yasiyoruhusiwa

Ukigundua kwamba kuna taarifa ambazo zimetumwa kwa BibleProject kwa njia isiyoruhusiwa, ikiwa ni pamoja na taarifa za watoto, tafadhali tujulishe kwa kuwasiliana nasi kwa kutumia maelezo ya mawasiliano yaliyoorodheshwa hapa chini ili tuzifute.

Maelezo ya Mawasiliano

Katika kutumia haki zako zozote za Taarifa zako za Kibinafsi, kuuliza maswali kuhusu utaratibu wa kukusanya na matumizi ya Taarifa zako za Kibinafsi au kutoa maoni kuhusu Sera hii ya Faragha na taratibu zetu za faragha, tafadhali wasiliana nasi kupitia:

Piga Simu Bila Malipo: (855) 700-9109

Barua pepe: webmaster@bibleproject.com

 

By using this website, I acknowledge that I am 16 years of age or older, and I agree to the Terms and Conditions and Privacy Policy.
Under 16?
Accept
For advanced bible reading tools:
Login  or  Join
Which language would you like?